Mrejesho toka kwa viongozi wa maeneo tuliyofanyia utafiti

Miongoni mwa mambo ambayo ni ya msing katika utafiti huu wa kuifahamu hali ya maendeleo ya vijana ni pamoja na kujua wadau mbalimbali wa vijana na masuala ya vijana wanavyoifahamu hali hiyo na kwa namna gani wangewazungumzia vijana.

Hapa inapelekea sisi watafiti katika utafiti huu kuweza kuwashirikisha viongozi wa serikali katika ngazi ya maeneo husika tuliyofanyia utafiti mara baada tu ya kumaliza kukusanya taarifa zinazowahusu vijana wa maeneo hayo. Hii imetupa fursa ya kuweza kuwaeleza walau kwa kifupi viongozi wa maeneo hayo husika ni kwa namna gani vijana wanazungumzia hali yao ya maendeleo hasa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita yaani miezi kumi na miwili katika mwaka 2012.

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuweza kujua vijana wanajishughulisha vipi katika shughuli za kiuchumi kujiingizia kipato na kwamba kama ipo mifumo sahihi ya kuwawezesha kufanya hivyo. Jambo jingine ni nmna wanavyoshiriki katikaq masuala ya uongozi au yale yanayoibukia katika jamii.

Changamoto

Miongoni mwa changamoto zinazotukumba ni pamoja na muda uliotengwa kwa ajili ya kufanya utafiti katika maeneo husika kuwa finyu kiasi cha kukosekana muda wa kutosha kuweza kuwapa mrejesho viongozi husika. Tunalazimika kuondoka pale siku ya mwisho kukusanya data inapoishia.

Vilevile viongozi wengi katika wilaya husika hawako tayari kutupa muda wa kuzungumza nao juu ya tulichokigundua miongoni mwa vijana huku wengine hawapatikani kabisa hata kuweza kuweka miadi na kuzungumza nao.

Tumelazimika mara nyingi kutumia simu kuweza kuwaeleza walau kwa kifupi juu ya hali ya maendeleo ya vijana kutokana na changamoto hiyo ya muda. Wengi wanaahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kwamba wangependa kuiona ripoti itakayoeleza vijana wa maeneo mengine wanasemaje juu ya hali zao ili waweze kupanga mikakatti itakayowagusa na kuiboresha hali ya vijana.

“Nashukuru kama mmefanikisha kuonana na vijana wa hapa, naamini wamewaeleza kinagaubaga juu ya hali yao, ningependa kuwaomba mtusaidie pia kuwapa elimu na kutuletea pia wale waliyoyasea wenzao…” anasema Bi Anne Julius, Afisa Mtendaji Old Sumbawanga

Advertisements
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

3 Responses to Mrejesho toka kwa viongozi wa maeneo tuliyofanyia utafiti

  1. Pingback: Are we integrating ICT, buy-in and transparency in research processes? The case of “The state of youth study” in Tanzania. | Today in Tanzania

  2. Pingback: Integrating ICT into research design - Research to Action - Research to Action

  3. Pingback: Integrating ICT during the research design phase - Research to Action - Research to Action

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s